![]()
Wanawake
Kundi la Wanawake la Barza la Wakimbizi la Uskochi (Scottish Refugees Council's Women's Group)
Ikiwa wewe ni mkimbizi wa kike unayeishi Glasgow basi kwa nini usije kwa kundi la Wanawake Jumatatu mchana. Sisi ni kundi la usaidizi ambalo hutoa misaada ya kihisia na kijamii kwa wakimbizi wa kike na watoto wao. Shabaha ya kundi hili ni kutoa mazingira safi na ya kupendeza ambako mchango wa kila mmoja unathaminiwa. Kila mara tunatarajia kupata wanawake wapya kujiunga nasi na kushiriki katika shughuli zetu au hata kuonana na wanawake wengine, kunywa kikombe cha chai na pia kupata chakula.
Kundi hili hukutana katika Quaker Meeting House Elmbank Crescent (upande wa pili wa Charing Cross Station na nyuma ya ukumbi wa Kings Theatre katika mtaa wa Bath Street) kila Jumatatu mchana kuanzia saa 08:00 mchana hadi saa 11:00 jioni..
Kwa maelezo zaidi piga simu yetu ya bure nambari 0800 085 6087 au ufike tu.
Kuna mashirika mengi mazuri ambayo hushughulikia wanawake pekee hapa Uskochi.
Nenda kwa Mawasiliano ya Kufaa kupata maelezo juu ya mashirika haya.
Maelezo Zaidi ya Mawasiliano
Afya ya wanawake yaweza kuathiriwa na vitu vingi, kwa mfano, mpangilio wa chakula, afya na mambo mabaya ambayo yametukia. Kijitabu hiki kinakueleza la kufanya endapo unajikuta katika hali hiyo:
Hatuwezi kuthibitisha kwamba maelezo yote yaliyoko katika ukurasa huu yametafsiriwa katika lugha yako. Ikiwa unataka usaidizi au maelezo zaidi tafadhali wasiliana na Scottish Refugee Council simu nambari 0800 085 6087
