![]()
Usafiri Glasgow
Mabasi
Mabasi ni usafiri wa rahisi zaidi kote katika Uskochi. Kuwahi basi huko Glasgow lazima uende kwa kituo cha basi ambacho kinaonyesha nambari ya basi unayotaka kuingia. Mara nyingi itakuwa rahisi ikiwa utanyosha mkono ili dereva wa basi aweze kuona ungelitaka basi lisimame kwa ajili yako.
Pesa unazomlipa dereva huitwa 'nauli ya basi'. Mabasi mengi hayarejeshi pesa zilizolipwa zaidi kwa hiyo lazima ujaribu kutoa kiasi cha sawa cha nauli. Watoto wa hadi kufikia umri wa miaka 5 husafiri bure. Watoto wa umri wa kutokea miaka 5 hadi 6 hulipa nauli ya chini kidogo. Unaweza kununua tiketi ya safari za kwenda na kurudi. Ikiwa hutumia sana usafiri wa basi, ingelikuwa jambo la busara kununua kadi ya usafiri ya wiki moja au mwezi mmoja. Unaweza kupata kadi hizi katika Kituo cha Usafiri. Unaweza kupata maelezo juu ya nambari za mabasi, bei, nambari na masaa katika Kituo cha Mabasi cha barabara ya Buchanan Street na Kituo cha Usafiri cha St. Enochs Travel Centre.
Hapa kuna viungo kwa ruti muhimu za basi katika mji wa Glasgow:
Ruti 62 - Faifley - Clydebank - Scotstoun - Partick - City centre - Parkhead - Shettleston - Baillieston
Ruti 75 - Milton - Ashfield - Possilpark - City Centre - Gorbals - Kings Park - Castlemilk
Ruti 12 - Woodhill - Auchinairn - Balornock East - Barmulloch - Barnhill - Sighthill - City Centre - Gorbals - Polmadie - Rutherglen
Ruti 45 - Woodhill - Stobhill Hospital - Springburn - Sighthill - City Centre - Queens Park - Shawlands - Thorliebank
Treni
Vituo viwili muhimu vya treni mjini Glasgow ni Queen Street na Central station.
Treni za nchi nzima au za maeneo ya karibu zote huondoka kutoka vituo hivi.
Hapa kuna ramani ya ruti zote za treni mjini Glasgow.
Subway
Subway ni huduma ya reli ya chini ya ardhi ambayo inapitia eneo lote la kati mjini Glasgow. Kabla ya kuingia Subway lazima ununue tiketi yako kutoka kwa ofisi ya uuzaji tiketi au kutoka kwa moja ya mashine za tiketi kituoni.
Subway hutumika Jumatatu hadi Jumamosi saa 12:30asb. - 05:00usiku na Jumapili kutoka saa 05:00asb - 12:00jn.
Ramani hii inaonyesha ruti ya subay mjini Glasgow.
Maelezo ya Viungo zaidi
Angalia mtandao huu kwa maelezo zaidi juu ya masaa ya basi na bei za basi mjini Glasgow. Unaweza pia kupata maelezo haya katika Kituo cha Basi cha Buchanan Street Bus Station, St.Enochs Travel Centre au piga simu ya kuuliza (SPT enquiry line on 0870 608 2608).
Maelezo ya Treni za eneo au Nchi nzima
Mtandao huu unakupa maelezo juu ya masaa ya treni na bei zake.
Hatuwezi kuthibitisha kwamba maelezo yote yaliyoko katika ukurasa huu yametafsiriwa katika lugha yako. Ikiwa unataka usaidizi au maelezo zaidi tafadhali wasiliana na Scottish Refugee Council simu nambari 0800 085 6087
