Return to graphical site

Scottish Refugee Council

21st August 2008
Advice in your language: English French Farsi Arabic Kurdish Somali Swahili Turkish Urdu
You are here: Home » Advice » Swahili » Money

*

Pesa

Baraza la Ukimbizi Uskochi (Scottish Refugee Council) laweza kukushauri wewe juu ya matatizo ya pesa. Kwa mfano tunaweza kukusaidia kujaza fomu yako ya maombi ya misaada ya kijamii kutoka kwa shirika la Taifa la Huduma za Usaidizi kwa Wakimbizi {National Asylum Support Service (NASS)} wakati unatafuta Ukimbizi au kukufahamisha jinsi ya kudai malipo yako ya kijamii ikiwa umeisha kubaliwa kuwa mkimbizi.

Mawasiliano Zaidi ya Maelezo

Unaomba msaada wa Ukimbizit (Septemba 2004)

Watafutaji Ukumbizi hawaruhusiwi kuajiriwa. Kwa kuwa utaratibu wa kuomba ukimbizi waweza kuchukua muda mrefu lazima ufikirie jinsi utakavyo jikithi maisha yako. Huenda ukakubaliwa kuwasilisha maombi ya msaada kutoka kwa Shirika la Taifa la Huduma za Usaidizi wa {National Asylum Support Service (NASS)} Kijitabu hiki kilitolewa pamoja na Baraza la Ukimbizi la England (Refugee Council in England).

Jamaa wako wamekatazwa kuwa wakimbizi? (Novemba 2004)

Jee! wewe na jamaa wako mmekatazwa ukimbizi? Umepokea barua kutoka kwa Wizara ya Ndani (Home Office) iitwayo '? 'Hali yako nchini Uingereza na Kifungo cha 3 cha sheria ya Uraia, Uhamiaji na Ukimbizi ya mwaka 2002' Kijitabu hiki kimetolewa na Baraza la Ukimbizi na Tendo la Ukimbizi (Refugee Council and Refugee Action).

Wewe ni raia wa Iraq ambaye umefikia mwisho wa utaratibu wa kuomba ukimbizi re? (Febuari 2005)

Ikiwa Wizara ya Ndani imekataa maombi yako ns kisha umeshindwa katika rufaa ya maombi yako ya ukimbizi, basi yselekea kwamba msaad wako kutoka Huduma ya Taifa ya Msaada kwa {National Asylum Support Service (NASS)} nao pia umesimamishwa.

Halmashauri ya Ushauri kwa Raiau

Halamashauri ya Ushauri kwa Raia (Citizens Advice Bureau) hutoa ushauri juu ya pesa, nyumba na maswala mengine yanayohusiana na haki zako. Angalia katika mtandao huu kupata ofisi ya ushauri ilioyo karibu nawe. Mtandao huu una maana zaidi kwa watu ambao wameishakubaliwa kuwa Wakimbizi na wangelitaka kujua haki zao.

Hatuwezi kuthibitisha kwamba maelezo yote yaliyoko katika ukurasa huu yametafsiriwa katika lugha yako. Ikiwa unataka usaidizi au maelezo zaidi tafadhali wasiliana na Scottish Refugee Council simu nambari 0800 085 6087.

Rejea kwa Menyu muhimu ya Ushauri