Return to graphical site

Scottish Refugee Council

21st August 2008
Advice in your language: English French Farsi Arabic Kurdish Somali Swahili Turkish Urdu
You are here: Home » Advice » Swahili » Legal

*

Kisheria

Ni muhimu sana kwamba wewe uwe na wakili aliyefuzu (wakili wa kisheria) akupe ushauri juu ya maombi yako ya ukimbizi. Baraza la Ukimbizi Uskochi (Scottish Refugee Council) laweza kukuelekeza kwa Mawakili wa sheria ya ukimbizi katika Uskochi. Unaweza pia kutafuta mawakili waliofuzu katika mtandao Mtandao wa Chama cha Sheria cha Uskochi (Mtandao huu unapatikana kwa lugha ya Kiingereza pekee)

Ikiwa ungelitaka kusoma zaidi juu ya swala hili la utaratibu wa kisheria juu ya watafutaji ukimbizi nchini Uingereza basi nenda kwa sehemu ya 'Maelezo' ya mtandao huu.


Maelezo Zaidi ya Mawasiliano

Ofisi ya Kamishna wa Huduma za Uhamiaji (Office of the Immigration Services Commissioner (OISC)

Ofisi ya Kamishna wa Huduma za Uhamiaji (OISC) ina wajibu wa kuhakikisha kwamba washauri wote wa maswala ya uhamiaji wanatoia huduma za haki. Ikiwa ungelitaka kulalamika juu ya wakili wako, basi wasiliana na OISC.

Hatuwezi kuthibitisha kwamba maelezo yote yaliyoko katika ukurasa huu yametafsiriwa katika lugha yako. Ikiwa unataka usaidizi au maelezo zaidi tafadhali wasiliana na Scottish Refugee Council simu nambari 0800 085 6087.

Rejea kwa Menyu muhimu ya Ushauri