Return to graphical site

Scottish Refugee Council

21st August 2008
Advice in your language: English French Farsi Arabic Kurdish Somali Swahili Turkish Urdu
You are here: Home » Advice » Swahili » Housing and Welfare

*

Makaazi & Kijamii

Jee Unapata usaidizi wa NASS?

Ikiwa wewe umepelekwa Glasgow kutoka England na serikali ya Uingereza utapokea usaidizi wako kutoka kwa shirika la serikali liitwalo National Asylum Support Service (NASS).

Ikiwa una tatizo lolote na nyumba yako, kwa mfano majirani wabaya, uchafu, vifaa vya umeme vya kuvunjika lazima uwasiliane na Ofisa wa Mradi wako kwa kutumia nambari ya simu uliyopewa wakati ulipoingia nyumba yako.

Ikiwa bao unaendelea kupata matatizo basi unaweza kuwasiliana na Mradi wa Usaidizi wa Watafutaji Ukimbizi au (Asylum Seeker Support Project) nambari ya simu 0141 222 7300. Ikiwa tatizo hilo litaendelea basi wasiliana na Baraza la Ukimbizi la Uskochi (Scottish Refugee Council) nambari yetu ya simu ya bure ni 0800 085 6087.

Ikiwa wewe ni mtafutaji ukimbizi ambaye hupati msaada wa NASS?

Ikiwa umewasilisha ombi lako la kutafuta ukimbizi na hupati msaada wa NASS basi Baraza la Ukimbizi Uskochi (Scottish Refugee Council) litapanga upate makaazi ya muda katika YMCA Glasgow hadi makaazi ya NASS yatakapo pangwa. Usaidizi na ushauri utatolewa juu ya kufikia msaada wa NASS, uwakilishi wa kisheria na huduma za afya.

Kwa Watu ambao wamekubaliwa Ukimbizi

Ikiwa umekubaliwa ukimbizi, basi una muda wa siku 28 kuondoka makaazi yako ya Huduma ya Taifa ya Usaidizi wa Wakimbizi {National Asylum Support Service (NASS)}. Hii inaweza kuwa na utaratibu mrefu kwa hiyo ni muhimu kwamba upate ushuari mara moja kutoka kutoka Baraza la Ukimbzi Uskochi (Scottish Refugee Council).

Baraza la Ukimbizi Uskochi (Scottish Refugee Council) laweza kukupa ushauri juu ya maswala yote ya nyumba, kama vile jinsi ya kuwasilisha maombi kwa chama cha nyumba au baraza, kukodisha nyumba kutoka kwa wenye nyumbza za kibinafsi, kutia fanicha katika nyumba yako mpya au hata kuhamia eneo jingine. Tunaweza pia kukushauri jinsi ya kupata ufadhili wa kijamii. Kwa kupanga mihadi katika ofisi yetu ya Glasgow au Edinburgh tafadhali piga simu yetu ya bure nambari 0800 085 6087.

Maelezo Zaidi ya Mawasiliano

Wewe u fukara na umefikia mwisho wa utaratibu wa kutafuta ukimbizi? (Ogasti 2004)

Kijitabu cha kukueleza njia mbali-mbali zilizoko ikiwa umefadhaika na mnamo mwisho wa utaratibu wa kutafuta ukimbizi?

Hatuwezi kuthibitisha kwamba maelezo yote yaliyoko katika ukurasa huu yametafsiriwa katika lugha yako. Ikiwa unataka usaidizi au maelezo zaidi tafadhali wasiliana na Scottish Refugee Council simu nambari 0800 085 6087

Rejea kwa menu muhimu ya Ushauri