Return to graphical site

Scottish Refugee Council

28th August 2008
Advice in your language: English French Farsi Arabic Kurdish Somali Swahili Turkish Urdu
You are here: Home » Advice » Swahili » Health

*

Afya

Ikiwa ombi lako la kutafuta ukimbizi linafikiriwa bado, (hii ni pamoja na rufaa) una haki ya kupata matibabu kutoka kwa Huduma ya Taifa Ya Afya {National Health Service (NHS)}.

Baada ya kuwasili katika makaazi yako utapewa barua inayokualika ujiandikishe kwa daktari wa eneo lako. Ikiwa unapata matatizo ya kujiandikisha kwa daktari tafadhali wasiliana na afisa wa mradi wako katika Baraza la Ukimbizi Uskochi (Scottish Refugee Council).

Ikiwa unapata msaada kutoka kwa Shirika la Taifa la Huduma za Ukimbizi {National Asylum Support Service (NASS)} watakupa hati ya HC2 ambayo unaweza kuiwasilisha kwa daktari kama waraka rasmi. Ikiwa hupati msaada kutoka kwa NASS utalazimika kujaza hati ya HC1 ili uweze kupata huduma za utunzi wa afya.

Wakimbizi (watu waliokubaliwa kuishi nchini) wana haki sawa ya utunzi wa afya kama raia yeyote wa Uingereza.

Daktari wako anaweza pia kuzungumza na wewe juu ya tatizo lolote la hisia ya akili ambayo inakukabili wewe: ikiwa unajisikia umefadhaika, upweke au kitu chochote kilichokupata ambacho unaona vigumu kukizungumzia. Daktari wako anaweza kukuelekeza kwa wataalamu ambao wamefundishwa kukusaidia na hali yako.

Maelezo Zaidi ya Mawasiliano

Afya Yako

Kijitabu hiki kinaeleza umuhimu wa kupata daktari katika eneo lako na ni wakati gani unaofaa kwenda hospitali.

Virusi vya HIV - Ukweli Wenyewe

Kijitabu hiki kinaeleza ni nini Virusi vya HIV na kitakuelekeza kwa mashirika hapa Uskochi ambayo hupima virusi na kutoa usaidizi kwa watu walio na shida hiyo.

Hatuwezi kuthibitisha kwamba maelezo yote yaliyoko katika ukurasa huu yametafsiriwa katika lugha yako. Ikiwa unataka usaidizi au maelezo zaidi tafadhali wasiliana na Scottish Refugee Council simu nambari 0800 085 6087.

Rejea kwa menyu muhimu ya Ushauri