![]()
Elimu na Uajiri
Watoto
Elimu kwa Watoto waliofikisha umri wa kwenda Shule ni bure nchini Uingereza na kufuatia sheria watoto wenye umri wa kati ya miaka 5 hadi 16 lazima wahudhurie shule. Watoto wote wa Watu wanaotafuta Ukimbizi na Wakimbizi pia wana haki ya kupata elimu ya bure na wanachukuliwa kuwa sawa na watoto wengine wote.
Elimu na Uajiri kwa Watu wazima
Baraza la Ukimbizi la Uskochi hutoa maelezo na maelekezo ya kibinafsi na kwa siri juu ya taaluma.
Hii ni pamoja na:
* Ushauri juu ya elimu, mafunzo, uajiri na kazi za kujitolea..
* Majadiliano ya mmoja kwa mmoja juu ya taaluma yako upendayo na kugundua kozi zifaazo.
* Ushauri juu ya misaada ya masomo kwa mafunzo ikiwa ni pamoja na ada ya mafundisho na misaada ya wanafunzi.
* Usaidizi wa kutafuta kazi ikiwa ni pamoja na kutayarisha mitalaa ya masomo na ujuzi, barua za maombi ya uajiri na uandalizi wa mahojiano.
* Msaada wa uandikishaji wa ujuzi wa ng'ambo na jinsi ya kufikia takwimu za NARIC na utafsiri wa hati, na diploma.
Kwa kupanga mihadi katika ofisi zetu za Glasgow au Edinburgh tafadhali piga simu yetu ya bure nambari 0800 085 6087. Lau sivyo, unaweza kufika na kuhudhuria Vikao vya Ushauri juu ya Elimu na Uajiri (Education and Employment Advice Sessions) vya Glasgow au Edinburgh:
| Kikao cha Ushauri | Lini | Wapi |
| Edinburgh | Alhamisi 13:00 - 16:00 | Edinburgh Refugee Centre,St, Georges West, 58 Shandwick Place, Edinburgh |
| Glasgow | Jumatano 10:00 - 13:00 14:00 - 16:00 |
Scottish Refugee Council, 5 Cadogan Square (end of Cadogan Street), Glasgow |
Maelezo Zaidi ya Mawasiliano
Maelezo juu ya kozi za Koleji na Vyuo vikuu zinazopatikana Uskochi.
Okoa Watoto (Save the Children)
Mtandao huu unatoa maelezo mazuri kuhusiana na elimu ya watoto wako.
Elimu na kujiandaa kwa Ajira (Education and Preparation for Employment).
Wewe ni mtafutaji Ukimbizi unayeangalia maelezo juu ya elimu au kujiandaa kwa ajira? Mtandao huu una maelezo ya kina, sehemu za kuwasiliana na njia za kuweza kupata kusoma. Kuna maelezo kwa Muhtasari kwa lugha 8.
Kiingereza kwa Watu wanao ongea Lugha Nyingine ESOL (English to Speakers of Other Languages)
Mtandao huu una daftari ya orodha ya mashirika, koleji na mashirika ya kujitolea yanayotoa masomo ya Kiingereza kwa Watu wanao ongea Lugha Nyingine {English for Speakers of Other Languages (ESOL)}. Daftari hii ina zaidi ya mashirika 60 ya madarasa ya lugha ya Kiingereza katika eneo zima la Greater Glasgow.
Hatuwezi kuthibitisha kwamba maelezo yote yaliyoko katika ukurasa huu yametafsiriwa katika lugha yako. Ikiwa unataka usaidizi au maelezo zaidi tafadhali wasiliana na Scottish Refugee Council simu nambari 0800 085 6087
