![]()
Kizuizini
Maafisa wa Uhamiaji nchini Uingereza, wamepewa uwezo mkubwa wa kuwazuilia watu kwa sababu za uhamiaji. Ni muhimu sana kupata wakili wa kisheria ambaye ataweza kukupatia ushauri ufaao juu ya kuzuiliwa kwako na kesi yako ya kujihami.
Wageni Wanaozuiliwa Uskochi (Scottish Detainee Visitors)
Wageni wanaozuiliwa Uskochi {Scottish Detainee Visitors (SDV)} hili ni shirika la misaada linalojitegemea linalotoa usaidizi wa kijamii, kihisia na kwa vitendo kwa wahamiaji waliozuiliwa Uskochi, hasa katika kambi ya Dungavel Immigration Removal Centre. Maafisa wa kujitolea wa SDV hutembelea Dungavel mara mbili kwa wiki siku za Jumatatu jioni na Alhamisi jioni.
Ikiwa umezuiliwa au unafahamu juu ya mtu yeyote aliyezuiliwa, na huenda akafaidi kutokana na kutembelewa, tafadhai wasiliana na Shirika la Wageni Wanaozuiliwa Uskochi (Scottish Detainee Visitors) kwa mtandao huu coordinator@sdv.org.uk, au kwa kupiga simu nambari 0141 248 9799 siku ya Jumatano asubuhi, au wakati wowote siku ya Ijumaa.
Maelezo Zaidi ya Mawasiliano
Ushauri wa Kisheria kwa Watu Ambao Wamezuiliwa na Idara ya Huduma za Uhamiaji.
Mtandao wa The 'MultiKulti' unakueleza haki zako endapo unatiwa kizuizini.
Usaidizi kwa Wahamiaji waliozuiliwa. (Kiingereza pekee)
Dhamana kwa Wahamiaji Waliozuiliwa {Bail for Immigration Detainees (BID)} hutoa ushauri kwa wahamiaji waliozuiliwa juu ya kupinga kuzuiliwa kwao.
Hatuwezi kuthibitisha kwamba maelezo yote yaliyoko katika ukurasa huu yametafsiriwa katika lugha yako. Ikiwa unataka usaidizi au maelezo zaidi tafadhali wasiliana na Scottish Refugee Council simu nambari 0800 085 6087.
